Tangazo la Nusura

Mara nyingine uzuri huzaliwa kwenye mazingira yasiyopendeza na yenye hali inayochukiza. Lakini wanaume hawaoni ni wapi uzuri ule ulikopaliliwa, jinsi gani ulivyochomoza na kunawiri pamoja na matatizo yote. Wanaona tu umbo lake, na kutaka kulimiliki. Siku zote Nusura alikuwa ni ‘malaika’ wa Duma; na kama walivyo malaika wote, yuko pale kulindwa na kutunzwa, lakini ukimtusi au ukimdharau kuwa wa kawaida tu, siku moja atajirukia apae. Hadithi ya Nusura ni ya ujasiri na yenye kuonya  ulimwenguni  ambapo wanaume wanaweza kudharau thamani ya ustahamilivu wa mwanamke.

 

Maoni: