Tangazo la Mzee Kizito

Ni mkuu wa familia, mzee wa mitala, kiongozi wa milki yake. Kama una tatizo la gari, basi hakuna sehemu bora ya kurekebisha vitu zaidi ya karakana ya Kizito. Yule pale, anaonekana zaidi kama daktari wa upasuaji kuliko nyani wa grisi. Na nyumbani, mzee Kizito, mwenye wake watatu na watoto kumi na saba, anaongoza nyumba isiyotetereka,  inayohusudiwa na jamii yake. Yeye ni kiongozi. Anapenda utamaduni, hasa muziki wa Taarab. Ana kila kitu. Ama sivyo? Vipi mzee Kizito ghafla amejikuta ana mambo mengi ya kuyasimamia…na atajimudu vipi pale mambo yatakapoanza kusambaratika?

 

Maoni: