Tangazo la Duma

Vijana watanashati kama Duma, ni matatizo, hasa pale, wanaposhindwa kukataa. Duma ana kila aina ya mabibi ambao angeweza akawa nao….isipokuwa malaika mmoja ambaye angekuwa naye maisha. Alijaaliwa kuwa na vitu vingi: uzuri, ucheshi, afya, ulimi mwepesi, na uwezo wa kuwemo katika hali yoyote, kuanzia geto mpaka maisha ya juu. Sasa kwa nini hataki kutulia? Kitu gani kinachomsumbua rohoni mwake kinachomzuia asiweze kupata penzi analolihitaji zaidi ya kitu kingine? Mwisho wa siku, pasi na uongozi wa wazazi wake, anaye mdogo wake, Stephen, anayelaziika kumwangalia.- hivyo hataki utani na mtu!

 

Maoni: