Tangazo la Cheche

Cheche – mpigapicha, ni mtawala wa maisha yake. Kwenye studio yake ya Mtungi, Cheche anaiweka jamii pamoja kupitia picha — familia, marafiki, wapweke na wapendanao wote wanamkabili kupitia lenzi ya kamera yake. Macho yao yanaeleza mengi kuhusu maisha yao, nafsi zao. Hakuna anachokipenda zaidi ya kuwafanya wateja wake watabasamu. Anafurahi sana anapowapa fursa ya kuota ndoto na kujipigia taswira ya jinsi gani wanataka waonekane.  Lakini kuna zaidi katika maisha kuliko kufurahi na kucheza. Tamaa ya jicho la Cheche kwa wanawake inaweza pia kumletea matatizo ya kila aina — hasa anapofahamu wazi kuwa ni lazima arudi nyumbani kwa mkewe mjamzito na watoto wake wawili wadogo.

 

Maoni: