Siri ya Mtungi – Sehemu ya 9

Kupotea kwa pikipiki yake nje ya nyumba ya ufukweni ya Lulu kunamfanya mpiga picha Cheche kuchanganyikiwa. Itakuwaje kama Cheusi atagundua uhusiano wake na Lulu? Cheche anarundika oungo juu ya uongo. Dafu anaahidi kumsaidia kuitafuta pikipiki — lakini kwa sababu tu anahisi kwa kufanya hivyo atakuwa karibu zaidi na Lulu.

Wakati huohuo, tangu Nusura alipoolewa na Mzee Kizito, Duma amekuwa hana uelekeo na maisha yake. Kovu anamtambulisha kwa mfanya biashara aitwaye Golden kule kwenye kigrosari cha Tula. Lakini Kovu anapolewa na kumtukana bibi yule, Duma anamgeuka na kumtetea Tula — kitu kinachomfanya yeye na Tula wagundue kuwa wana mambo yanayofanana.

Duma hana wasaa wa kukaa nyumbani, na muda si mrefu mdogo wake, Stephen, anachoshwa na masomo na kuelekea maskani kukutana na Max.

———-

The disappearance of Cheche’s motorbike from outside Lulu’s beach house causes the photographer to panic. What if Cheusi finds out about his affair with Lulu? Cheche piles on lies upon lies. Dafu offers to help him find the motorbike — but only because he thinks it might get him closer to Lulu.

Meantime, since Nusura married Mzee Kizito, Duma has been at a loss what to do with his life. Kovu introduces him to a businessman, Golden down at Tula’s kigrosari. But when Kovu gets drunk and insults the lady, Duma defends Tula — and he and Tula discover they share something in common.

Duma spends less time at home, and pretty soon his young brother, Stephen, gets tired of his studies and heads for the msakani to meet Max.

 

Maoni: