Siri ya Mtungi – Sehemu ya 6

Cheche anakwenda kufanya kazi ya binafsi ya kupiga picha akiambatana na Lulu, bila ya msaidizi wake, Shoti. Safari ya kikazi ya Cheche inaishia kwenye nyumba ya ufukweni ya Lulu. Cheusi, akihisi kuzidi kutengwa na mumewe, anamgeukia mama yake Mwanaidi kwa ushauri juu ya ndoa na familia.

Mtanziko wa Nusura unazidi kuwa mbaya. Shogake mpenzi, Julietta anamshauri, lakini Nusura ana mambo mengi maishani mwake ambayo hayajafumbuliwa. Kwa ghadhabu anamkabili baba yake, Masharubu, kuhusu mahari yaliyoahidiwa na Mzee Kizito. Moyo wake umegawanyika. Je, bado anampenda Duma au kuna uwezekano wa kuwa na maisha ya baadae na Mzee Kizito?

—————————-

Cheche goes on a photographic private assignment with Lulu without his assistant, Shoti. He ends up at her beach house. Cheusi, feeling more and more neglected by her husband, turns to Mwanaidi for advice on marriage and family.

Nusura’s dilemma just gets a whole lot worse. Her best friend, Julietta, advises her, but Nusura has many unresolved issues in her life. She furiously confronts her father, Masharubu, about a dowry promised by Mzee Kizito. Her heart is torn. Does she still love Duma or can there be a future with Mzee Kizito?

 

Maoni: