Siri ya Mtungi – Sehemu ya 14

Msimu wa kwanza ya tamthilia hii uilipokelewa vizuri sana kama namna nyingine ya kutoa hadithi mbalimbali zinazo zungumzia Waafrika. Msimu wa 2 utakuwa unaburudisha zaidi, wadhamini wameahidi hivyo. Siri ya Mtungi inaangazia waigizaji maarufu wa Kitanzania na pia imeleta vipaji vipya, hiki ni kitu kinachovutia na kufurahisha na wakati mwingine kinaangazia maisha ya kawaida ya watu wa pwani.

Kiini cha tamthilia hii ni Studio ya Mtungi ambapo uhusika wa Cheche – uliyochezwa na Juma – anatamaa ya kuwa na biashara yenye mafanikio ya kupiga picha. Kupitia lenzi yake, watazamaji wanakuwa karibu na wahusika katika jamii ya Cheche wakati yeye mwenyewe anapambana kusawazisha furaha ya nyumbani na msisimko ambao anaupata kutoka upigaji picha. Vilevile anatimiza furaha na ndoto za watu waliyomzunguka. Lakini je, anaweza kujitosheleza yeye mwenyewe?

Watazamaji wa msimu wa kwanza wa Siri ya Mtungi wataelewa zaidi hidithi ya Duma na Nusura, Wapenzi wawili ambao wametenganishwa kutokana na mazingira yao. Msimu wa pili unaangazia maisha ya hawa wapenzi katika njia tofauti. Duma anajiingiza katika mambo yakihalifu ili kujipatia pesa za haraka. Anasingizia kwamba kuchagua kwake kuishi hivi inatokana na yeye kutendewa vibaya na kutokuwa na chochote kingine cha kukifanya. Na Nusura anapata tumaini la kupata mapenzi ya dhati ya kumlinda mwanae anayetegemea kumleta katika dunia yenye changamoto nyingi sana. Ni hadithi yenye hisia kali ambayo itawavuta watazamaji.

Msimu wa pili pia unawaweka watazamaji kati kati kwenye maisha ya Mzee Kizito na muungano wa wake zake. Maisha yake yanafungwa anapobaini kuwa uamuzi wake wakumuowa mwanamke wa tatu Nusura, ulikuwa ni uamuzi usiye na fikra wa kutosha na hukuja kuvuruga mambo yake yeye na ya familia yake.

Kamera yetu itawaruhusu watazamaji wapite ukuta za manyumba, wapite milango iliyofungwa na kuwapa nafasi ya kusikia miguno ya mapenzi, na kupata ushahidi, kusikia uongo na ukweli, na maumivu ambayo hayajawahi kuonekana kwenye TV za Tanzania. Watu wanapambana kufikia maamuzi ya tamaa dhidi ya haja na kuhakikisha na kufurahisha maisha yao ili yawe sawa na huruma na wema kwa wote. Na katika maigizo ya wahusika wa kike, kama Mwanaidi na Farida, watazamaji wanatakiwa kugundua aina mpya ya uzuri na ukweli ambao unaenda zaidi ya muonekano wao wa nje.

Tamthilia ya Siri ya Mtungi inatumika kuleta matumaini na msukumo kwa watu wanao zungumza Kiswahili kwenye ulimwengu wa kiswahili kwa kuonyesha tabia za kipekee za watu wa Afrika ya Mashariki. Kupitia mchezo wa kuigiza, vichekesho na mengineyo, watengenezaji wa tamthilia hii wanakuletea ukweli na ufahamu katika uzoefu wa Kiafrika, kwa idadi kubwa ya watazamaji wa Afrika ambao wanataka kuona maisha yao wenyewe yakionyeshwa kwenye TV kwa upendo na kwa undani zaidi.

Swhailiwood Cheche Duma Africa TV television televisheni tamthilia filamu, Siri ya Mtungi,Swahili,Kiswahili,Tanzania,Africa,Drama,TV,Televisheni,television,soap,MFDI,ITV,EATV,Bongo,Filamu,Cheche,Lulu,Kizito,Duma,Episode,Sehemu,Tamthilia,Kenya,Uganda,Mozabique,Congo,Burundi,Monalisa,Yvonne Cherrie
SUBSCRIBE: http://goo.gl/cR0mA

 

One Response to Siri ya Mtungi – Sehemu ya 14

  1. BARAKA KALINGA says:

    Tamthilia hii ni bora kwa afrika, inaelimisha na imeakisi maisha ya kiafrika hasa tanzania

     

Maoni: