Roho ya Mapambano

Steps for the Future Presents: A Fighting Spirit (Kiswahili)

Shujaa wa taifa anageuka adui wa jamii pale anapoamua kutoboa siri yake. Gilbert Josamu, mwanamasumbwi bingwa wa uzito wa kati, aligundua kuwa ameathirika na VVU wakati akiwa kileleni mwa umaarufu wake. Akiwa anaishi katika jamii ambayo mtu kuwa na VVU ni kama dhambi isiyosameheka, Josamu anaamua kuendelea na ndondi bila kuweka wazi hali yake. Miezi michache kabla hajafariki, Josamu aliamua kuuweka wazi ukweli kuwa amekuwa akiishi na VVU kwa miaka 14. Hivyo pambano gumu kuzidi yote maishani mwake ndo linaanza — pambano la kusamehewa na kukubaliwa tena.

—————————

A national hero turns public enemy when he confesses his secret. Gilbert Josamu, Zimbabwean middle-weight boxing champion, discovered he was HIV positive at the height of his boxing career. Living in a society where HIV/AIDS is taboo, Josamu decided to pursue his career without disclosing his status. Just months before his death, he confessed to living with HIV for 14 years. Thus began his toughest battle yet- the battle for acceptance.

 

Maoni: