Kadi ya Njano

Tiyani yuko katika ukingo wa kuwa mcheza mpira maarufu – akiwa na miaka 17 tu! Kama nyota wa timu yake ya mpira ya Hyenas, mtoto mtiifu na kiranja shuleni kwake, Tiyani ana matarajio makubwa katika maisha yake.

Lakini msukosuko wa maisha, ujana, na mapenzi unauyumbisha mwelekeo wake. Kila mtu anahamu ya kumpata, hasa Linda, rafiki yake wa utotoni. Tiyani anajiingiza katika mapenzi, lakini hayuko tayari kwa matoeko yake, kama vile kupendana na msichana mwingine au kupata mtoto.

Kadi ya Njano ni filamu inayochekesha na ya kusisimua inayohusu mapenzi ya ujana, mpira wa miguu, naraha za maisha. Ndoto za kijana mmoja za kufanikiwa katika maisha.

 

Maoni: