Hadithi za Kumekucha: Tunu

Filamu ya Kumekucha – Tunu (Zawadi) ni hadithi ya Mashoto, ambaye anafanya kazi kama kondakta wa daladala mjini. Maisha ya Mashoto mjini ni ya upambanaji. Dar es salaam in maisha ya anasa, na Mashoto anapenda hivyo. Hana muda wa kufikiri juu ya watu na maisha aliyoyaacha kijijini, mpaka anapopata taarifa ya msiba wa mama yake.

Anaporudi nyumbani kwa ajili ya msiba, huzuni ya kumpoteza mama yake inamfanya achanganyikiwe. Anaamini ardhi imelaaniwa na hataki kusikia lolote kuhusu hiyo. Baba yake, Sanga anapoteza matumaini juu yake. Baada ya muda kidogo, anajikuta anafanya kazi na dalali mwenye dhuluma, Kidevu. Ni mapambano magumu kwa Mashoto, wakati anajitahidi kutafuta dhumuni ndani ya kijiji.

Lakini bado, mama yake amemuachia zawadi. Sauti yake, na uwepo wake usioonekana, sauti inayomuambia kwa upole afungue macho na kuzibua masikio yake, ili aweze kujifunza somo juu ya uoto wa asili wa dunia na mizizi itoayo rutuba kutoka kwenye hiyo.

Baada ya kufukuzwa nyumbani na baba yake kwa kutumia pesa kidogo alizoziacha mama yake, Mashoto lazima ajifunze kuishi kwa kutegemea ardhi. Lazima ajifunze jinsi ya kukabiliana na maadui wa zamani na kutafuta marafiki wapya. Lazima ajifunze kupambana na kupenda. Lakini jambo la muhimu zaidi, Mashoto lazima atambue kile anachokipigania.

Subscribe: http://goo.gl/cR0mA
Facebook: http://ift.tt/2A6nDNP

 

Maoni: